DEMOS POINT
Tuesday, December 28, 2010
Monday, December 13, 2010
Sunday, February 7, 2010
NANI WA KULAUMIWA KWA KUFELI KWA KISHINDO
Nimelazimika kutumia muda wangu huu mchache kujadili mambo machache lakini muhimu ili tuweze kumtambua adui yetu ni nani (machawi wetu anaetufanya tunakuwa na matokeo mabovu)
nimeamka asubuhi na mapema nikiwa najiandaa na shughuli zangu za kawaida ndipo nilipopata taarifa za kusikitisha kwamba matokeo kidato cha nne yatoka wanafunzi wamefeli kwa kishindo.
Binafsi naamini matoke mabovu ni pigo kubwa kwa wazazi wetu, walezi wetu,na hata bibi na babuzetu ambao wamekuwa wakitumia ghrama nyingi hata kuzitoa sadaka rasilimali zao ili kuhakikisha watoto wao, wajukuu zao,na majirani zao wanapata elimu ili kuja kuwakomboa katika lindi hili la umasikini.
Serikali nayo imeonyesha jitihada kubwa za kuhakikisha huyu mtanzania mtoto wa masikini na mfanyakazi anapata elimu ili kukidhi matakwa na malengo ya milenia. Kuhakikisha hili linafanyika serikali imeweza kuhamasisha ujenzi wa sekondari kila kata ambapo ilianza na sera ya MMEM huu ulikuwa mahususi kwa shule za msingi na baadae MMES uliolenga sana shule za sekundari. Ujenzi huu ulienda sambamba na kuwakandamiza watanzania,kuwanyanyasa kwani hapa ndipo pale watendaji walikabidhiwa rungu na waliweza kuwanyanganya hata kuku wale wazazi mafukara wa kutupa na kuwaita wao wanapinga maendeleo kwa wao kutoshiriki kuchangia. Hakuna ukweli kwamba hawa mafukara hawakupenda kuchangia ila ni hali ngumu ya maisha iliyowafanya washindwe kuchangia ujenzi wa shule hizo. Kwa kweli kilikuwa kipindi kigumu sana kwa wananchi hasa ukizingatia wananchi hawa wa Tanzaniani wanalipakodi ya maendeleo na moja ya kazi za kodi yao ni kuboresha huduma za kijamii mfano elimu,afya nk.
Baada ya mateso hayo wananchi waliamini sasa huu ni muda wa wao wa kupumua kwani walizingatia sana msemo wa kiswaili usemao baada ya dhiki ni faraja. Hali haikuwa kama walivyoamini kwani sasa imegeuka kuwa mbaya baada ya kuona lile tumaini lao linapotea. Watanzania wao wametimiza wajibu wao wakujenga shule. serikali vipi? waziri anatuambia nini watanzania? lazima tujue Bwana Maghembe na hao wataalamu wake wanafanya kazi gani mbona kila kukicha na tangu wao wawe mawaziri matokeo ni mabovu? Inakuwaje waziri awe profesa lakini anakuwa sehemu ya kuporomoka kwa elimu hii ya Tanzania.
tunaambiwa tusimtafute mchawi tuanzie hapo tulipoangukia lakini sasa nimeamua kabisa kumtafuta mchawi. Tatizo ni viongozi wetu hasa wa wizara husika. Nasisitiza wao ndio wachawi kutokana na majibu yao wanayoyatoa yasizokuwa na utafiti wowote wa kitaalam majibu yao ni kama utabiri wa waganga wapiga ramli. Wamekuwa wakitoa majibu ya kuwaridhisha watanzania tuu badala ya kuonyesha tatizo na kulitafutia ufumbuzi. majibu yao hawa mawaziri kuanzia waziri Maghembe ambae yeye ni prof hatofautiani na yale ya makamba ambae hatuzijui sifa zake za elimu. ni sawa kabisa na ya mama GHASIA na yale ya SOPHIA SIMBA yanayotolewa katika misingi ya kukomoa na kukomesha.
Kitendo cha kushindwa kuboresha mazingira ya walimu pamoja na maslai yao yote hii ni moja ya sababu ya vijanawetu kufeli.

Saturday, February 6, 2010
MAISHA YA MPAMBANAJI
Nimezaliwa mwaka 1984 katika kijiji cha Shiri Njoro Wilayani Hai mkoani kilimanjaro. Nimebahatika kusoma katika shule ya msingi Njoro niliposoma darasa la kwanza mpaka la saba na kujiunga na masomo ya secondari (Odinary level education) katika shule ya sekondari ya Hedaru iliyoko same mkoani kilimanjaro.mnamo mwaka 2001 hadi 2004 ambapo nilifanikiwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita(advanced education) mwaka 2005 hadi 2007 katika shule ya sekondari ya Kantalamba iliyoko mkoani Rukwa. Nilifanikiwa kufaulu vyema na mungu akanijalia kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2007 kama wanafunzi waanzilishi wa chuo hiki (THE PIONEER) na nipo chuo kiuu cha Dodoma nikiwa mwanafunzi wa shahada ya utawala wa umma niliebobea sana kwenye taaluma ya serikali za mitaa. (BACHELOR OF ARTS IN PUBLIC ADMINISTATION) nimeshiriki sana katika nafasi mbalimbali za uongozi nikiwa kama kiongozi wa wanafunzi tangu nikiwa darasa la nne sekondari na sasa nipo chuo kikuu. napenda sana kushiriki katiaka harakati za siasa hususani za kambi ya upinzani na kudhibitisha hilo nimekuwa mwana CHADEMA na sasa ni katibu wa CHADEMA vijana wilaya ya Hai.
Subscribe to:
Posts (Atom)