Saturday, February 6, 2010

MAISHA YA MPAMBANAJI

Nimezaliwa mwaka 1984 katika kijiji cha Shiri Njoro Wilayani Hai mkoani kilimanjaro. Nimebahatika kusoma katika shule ya msingi Njoro niliposoma darasa la kwanza mpaka la saba na kujiunga na masomo ya secondari (Odinary level education) katika shule ya sekondari ya Hedaru iliyoko same mkoani kilimanjaro.mnamo mwaka 2001 hadi 2004 ambapo nilifanikiwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita(advanced education) mwaka 2005 hadi 2007 katika shule ya sekondari ya Kantalamba iliyoko mkoani Rukwa. Nilifanikiwa kufaulu vyema na mungu akanijalia kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2007 kama wanafunzi waanzilishi wa chuo hiki (THE PIONEER) na nipo chuo kiuu cha Dodoma nikiwa mwanafunzi wa shahada ya utawala wa umma niliebobea sana kwenye taaluma ya serikali za mitaa. (BACHELOR OF ARTS IN PUBLIC ADMINISTATION) nimeshiriki sana katika nafasi mbalimbali za uongozi nikiwa kama kiongozi wa wanafunzi tangu nikiwa darasa la nne sekondari na sasa nipo chuo kikuu. napenda sana kushiriki katiaka harakati za siasa hususani za kambi ya upinzani na kudhibitisha hilo nimekuwa mwana CHADEMA na sasa ni katibu wa CHADEMA vijana wilaya ya Hai.

1 comment:

  1. how can your biography help us. keep on touch,it is just challenge. by mahenge.

    ReplyDelete